
Msanii wa kike nchini Maandy amewajibu wanaodai kuwa mafanikio yake kimuziki yametokana na yeye kutoka kimapenzi na maprodyuza wa muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram hitmaker huyo wa ngoma ya “By The Way” ameonakana kukasirishwa na wanaomema vibaya kwa kusema kwamba tuhuma hizo hazina ukweli wowote bali zimeibuliwa na watesi wake ambao wanalenga kumuharibia jina.
Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba kama kweliย angekuwa anajiuza kimwili kwa maprodyuza angeshapeleka muziki wake kimataifa kitambo.
“Huko clock app Wanasema Nagawa mbaya . If I was to use my body to get ahead , ningekua Grammies nikipigania space na Beyoncรฉ ,si hapa ungwaro ๐ฎโ๐จ๐ฎโ๐จ To the producers Iโve worked with kindly mark register hapa tuone mko wangapi ๐๐๐๐”, Aliandika Instagram.
Hii si mara ya kwanza kwa Maandy kuzushiwa taarifa za aina hii kwani kipindi cha nyuma alidaiwa kutoka kimapenzi na rapa Breeder LW, madai ambayo aliyakanusha vikali.