Maandy amvua nguo Dyana Cods kwenye wimbo mpya wa diss.
Rapa wa kike kutoka Kenya, Maandy, ameongeza moto kwenye bifu lake na Dyana Cods baada ya kuachia wimbo mpya wa diss unaoitwa “SideHü.” Wimbo huo, ambao umesambaa kwa kasi ya ajabu mitandaoni, unaonekana kuwa jibu la moja kwa moja kwa majigambo ya hivi karibuni ya Dyana Cods, ambaye alijitangaza kuwa mwandishi bora zaidi wa kike nchini Kenya na kupuuza uwezo wa wasanii wenzake. Katika kile kinachoonekana kama dharau ya kiwango cha juu, Maandy amemshambulia Dyana Cods kwa mistari inayokata kama wembe. Katika mstari mmoja unaozungumziwa zaidi, Maandy amesikika akisema, “Sikutambui, sikajui, sikuski,” kauli ambayo mashabiki wameifafanua kama mbinu ya kumshusha hadhi Dyana kwa kumfanya aonekane si chochote kwenye tasnia. Maandy ameenda mbali zaidi na kuhoji uwezo wa Dyana, akidai kuwa majigambo yake ya kuwa mwandishi bora hayana mashiko ikiwa hawezi kuonyesha kazi zinazokubalika na mashabiki wote.
Read More