Entertainment

Madonna atua mtaa wa Kibera nchini Kenya

Madonna atua mtaa wa Kibera nchini Kenya

Mwimbaji wa Marekani, Madonna ambaye tangu mwishoni mwa mwaka jana amekuwa katika ziara ya Krismasi barani Afrika, ametembelea mtaa wa mabanda wa Kibera jijini Nairobi nchini Kenya na kujumuika na watoto waliofurahia kukutana naye.

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 64 licha ya kuonekana mbichi alifurahia kazi ya Kennedy Odede, muasisi wa shirika lisilo la Kiserikali la SHOFCO ambalo hutoa huduma mbalimbali kwa watu wanaoishi mitaa ya kimaskini nchini Kenya.

Madonna alimsifia Odede kwa juhudi zake za kutoa huduma katika mitaa kama Kibera ikiwemo ni vyakula, elimu na maji kwa watu hao ambao hawana uwezo wa kumudu bidhaa hizo za kimsingi katika maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *