
Mahakama imemuagiza msanii Miss P kufuta video zote akimtuhumu Willy Paul kuwa alimdhulumu kimapenzi kwenye mtandao wa Youtube.
Kupitia nyaraka ambazo Willy Paul ameshare kwenye ukurasa wake wa Instagram mahakama imemtaka msanii huyo afute video hizo mara moja la sivyo atakabiliwa kisheria iwapo atakwenda kinyume na agizo la mahakama.
Ikumbukwe mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu Miss P alijitokeza kwa mara ya kwanza baada ya ukimya wa muda mrefu na kudai kwamba aliigura lebo ya Saldido kwa sababu Willy Paul alimnyanyasa kimapenzi. Jambo ambalo lilimfanya Willy Paul kufungua shauri mahakamani akidai kwamba Miss P alimuaharibi brand yake kwa kumzushia tuhuma za uongo.