Entertainment

Malenga mwenye asili ya wa Sudan Kusini akerwa na ubaguzi nchini Kenya

Malenga mwenye asili ya wa Sudan Kusini akerwa na ubaguzi nchini Kenya

Malenga maarufu mwenye asili ya Sudan, Ktwo amekanusha madai kuwa raia wa Sudan Kusini wanafadhiliwa na serikali yao kuishi nchini Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ktwo ameamua kutoa ya moyoni kwa kusema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote ikizingatiwa kuwa raia wa Sudan Kusini wanajitegemea wenyewe bila usaidizi wowote wa serikali.

Aidha amesema kasumba ya Wakenya kudhani kwamba raia wa Sudan Kusini wanalipwa kila mwezi kuishi humu nchini imepelekea wengi wao kubaguliwa wakiwa kwenye shughuli zao za kila siku hasa wanapofanya manunuzi ya bidhaa mbali mbali.

Hata hivyo amewataka wakenya kujitenga na mawazo hasi dhidi yao kwani raia wengi wa Sudan kusini wenye makaazi yao nchini Kenya wameathirika kisaikolojia kutoka na kauli za kibaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *