Entertainment

Mali za Tekashi 6ix9ine kupigwa mnada machi 5, 2025

Mali za Tekashi 6ix9ine kupigwa mnada machi 5, 2025

Mali na bidhaa za kifahari za rapa mtukutu kutoka nchini Marekani Tekashi 6ix9ine, ikiwa ni pamoja na vito, mabango ya muziki vinatarajiwa kupigwa mnada na Mamlaka ya huduma ya mapato nchini Marekani IRS ili kulipa madeni yake anayodaiwa.

Mnada huo uliopangwa kufanyika Machi 5, mwaka wa 2025, utakuwa na bidhaa za bei ya juu zilizonunuliwa na rapa 6ix9ine, ambazo baadhi zilionekana katika ngoma yake ya Gooba iliyotazamwa zaidi ya mara bilioni 1, ikiwemo cheni yake pendwa ya almasi yenye umbo la papa, inayotajwa kuwa na thamani ya zaidi shillingi millioni 7 za Kenya.

Mtandao wa TMZ umeripoti kwamba ukiona mpaka IRS wamefikia hatua ya kupiga mnada mali za rapa huyo basi huenda alikuwa akiandamwa na ukwepaji wa kodi kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *