LifeStyle

Malkia Karen Avishwa Pete ya Uchumba na Mpenzi Wake Zack

Malkia Karen Avishwa Pete ya Uchumba na Mpenzi Wake Zack

Mwanamuziki wa Bongofleva, Malkia Karen, ameanza ukurasa mpya maishani baada ya kuvalishwa pete ya uchumba na meneja wake, Zack, ambaye pia ni mpenzi wake wa muda mrefu. Tukio hilo limejiri baada ya miaka minane ya wawili hao kuwa kwenye mahusiano.

Katika video iliyoenea mitandaoni, Zack alionekana akimpelekea Malkia Karen zawadi maalum ikiwemo pete ya uchumba, kadi yenye ujumbe wa mapenzi na simu mpya aina ya iPhone 17. Wakati wa tukio hilo, Malkia Karen alikuwa gym, akishuhudia hatua hiyo ya kipekee kutoka kwa mpenzi wake.

Mashabiki wake wamefurahia tangazo hilo, wengi wakimpongeza kwa uvumilivu na safari ndefu ya mapenzi waliyoipitia na Zack. Tukio hili limeashiria mwanzo mpya wa maisha yao, huku ikitarajiwa sherehe kubwa ya harusi itakayofuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *