Gossip

Mama Dangote Adai Naseeb Junior Ndio Mrithi wa WCB Wasafi

Mama Dangote Adai Naseeb Junior Ndio Mrithi wa WCB Wasafi

Mama wa nyota wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, maarufu kama Mama Dangote, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kushiriki video ya mjukuu wake Naseeb Junior akiwa na baba yake katika ofisi za WCB Wasafi.

Katika video hiyo aliyoiposti Instagram, Mama Dangote ameandika maneno yanayoashiria kuwa huenda Naseeb akawa mrithi wa lebo ya WCB Wasafi, himaya ya muziki na biashara iliyoanzishwa na Diamond Platnumz.

Kitendo cha Mama Dangote pia kimeongeza tetesi za uwezekano wa Diamond na Tanasha kufufua tena mahusiano yao, kwani video hiyo imeonyesha namna mtoto wao anavyopata nafasi ya kipekee ndani ya ofisi za Wasafi, ikionekana kama ishara ya kuandaliwa kuchukua nafasi ya baba yake siku za usoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *