
Manchester United wanatayarisha ofa ya billioni 7.9 za Kenya kwa ajili ya kunasa saini ya mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Randal Kolo Muani.
Ripoti zinadai kwamba United hawako pekee yao kwenye mbio za kunasa saini ya Mshambuliaji huyo wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich
Hata hivyo Kolo Muani ambaye amejiunga na Frankfurt akitokea Nantes majira ya joto yaliyopita, inaaminika anatamani kubaki Frankfurt kwa sasa.
Bayern wamefanya mazungumzo na wawakilishi wake na wanadhamiria kumwacha Kolo Muani Frankfurt kwa muda wote uliosalia wa msimu huu, lakini bado hawajawasilisha ofa yao kama vile United wanavyoripotiwa kujiandaa kufanya hivyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ana mabao matano na pasi za mabao ‘assist’ nane hadi sasa katika msimu huu.