
Mastaa wa muziki wa Rap Nchini Octopizzo na Kayvo Kforce karibu warushiane makonde baada kuingia kwenye mzozo mkali huko Jiji Nairobi.
Rappers hao ambao walikutana uso kwa uso kwenye podcast ya mwafrika iitwayo Iko Nini wameonekana katika video wakipiga kelele na kutukanana wakati wakizuiwa na Walinzi wao.
Ikumbukwe Octopizzo na Kayvo Kforce wamekuwa katika bifu kwa wiki kadhaa sasa baada ya Kayvo Kforce kuikosoa album mpya ya rapa Octopizzo iitwayo Fuego kwa kusema kwamba ni album mbovu kuachiwa mwaka huu.
Hata hivyo jambo ambalo lilimfanya Octopizo kumkana Kayvo Kforce kwenye moja ya interview kwa kusema kwamba rapa huyo sio mzaliwa wa Kibera kwani tangu wafahamiane hajawahi jua maeneo ambayo anatokea.
Baada ya wawili kurushiana maneno makali Kayvo Kforce ameamua kuachia distrack iitwayo nyumba kumi ambayo amemvua nguo Octopizzo kwa kusema kwamba muziki wake umepoteza mvuto hivyo akome kutumia jina lake kujitafutia umaarufu.