
Wimbo wa Mariah Carey “All I Want for Christmas is You” umekuwa wimbo namba moja duniani baada ya kuvunja rekodi ya Spotify kwa kuwa na streams nyingi ndani ya saa 24. Ngoma hiyo imefanikiwa kufikisha streams zaidi ya milioni 21 siku ya krismasi kwa saa 24 tu
Sanjari na hilo Mariah Carey pia anaendelea kuvuna mabilioni ya fedha kupitia wimbo wake huo uliotoka mwaka 1994 ambapo kila mwisho wa mwaka kuelekea krismasi hujichukulia tena umaarufu duniani kote.
Kwa mujibu wa ripoti ya Economist, kila mwaka humuingizia Mariah Carey fedha za mirabaha dola milioni 2.5 ambayo ni zaidi ya shillingi millioni 307 za Kenya.