
Mwanamuziki kutoka Marekani Mariah Carey bado anaendelea kuweka rekodi mbali mbali kupitia wimbo wake wa “All I Want For Christmass is You” baada ya wimbo huo kukamata tena namba moja katika chati za Muziki za Billboard Hot 100 .
Wimbo huo ambao hutumiwa sana unapofika msimu wa Christmass,kwa mara ya kwanza mwaka 2017 uliingia Top 10 ya chati hizo, 2018 ukafanikiwa kuingia Top 5 na kisha kwa mfululizo ukakamata nafasi ya kwanza mwaka 2019, 2020 ,2021 na 2022 katika msimu wa Christmass.
“All I Want For Christmass is You” ambao ulitoka rasmi Oktoba mwaka 1994, uliandikwa na kutayarishwa na Mariah Carey pamoja na Walter Afanasieff.
Kwa mujibu wa ripoti ya Economist, kila mwaka humuingizia Mariah Carey fedha za mirabaha Dola milioni 2.5 ambayo ni zaidi ya Shillingi millioni 307 za Kenya.