Entertainment

Marioo Aendeleza Mafanikio ya The Goson Album kwa Toleo la Deluxe

Marioo Aendeleza Mafanikio ya The Goson Album kwa Toleo la Deluxe

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo, sasa anajiandaa kuachia rasmi Deluxe Edition ya albamu yake “The Goson”, ikiwa ni miezi saba imepita tangu atoe albamu yake hiyo iliyopata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki zake.

Kwa mujibu wa taarifa, Marioo ameongeza nyimbo kadhaa mpya kwenye toleo hilo maalum, hatua ambayo inalenga kuwapa mashabiki wake ladha zaidi ya kazi zake za kisanaa.

Ingawa hajatangaza rasmi orodha kamili ya nyimbo zitakazojumuishwa kwenye Deluxe, vyanzo vya karibu na msanii huyo vinaashiria kuwa baadhi ya nyimbo hizo tayari zimekamilika na zinasubiri muda sahihi wa kuachiwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Marioo kutumia mbinu ya Deluxe Edition. Wafuasi wake watakumbuka kuwa albamu yake ya awali, The Kid You Know, nayo ilipata toleo la Deluxe ambalo lilijumuisha vibao vipya kama Nikazama na Sing, ambavyo vilipata mapokezi makubwa.