
Kuizuia nyota ya Marioo ni sawa na kuziba mwanga kwa kiganja cha mkono. Nyota huyo kutoka Tanzania anaendelea kugonga vichwa vya habari na mara hii ni kuhusiana na idadi ya views youtube.
Good news kwa mashabiki wa mkali huyo ni kwamba amefikisha watu Milioni 100 waliotazama kazi zake mbalimbali katika channel yake ya mtandao wa Youtube.
Marioo alijiunga na mtandao huo Januari 4, mwaka wa 2018 na amepata watazamaji wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo.
Baadhi ya matukio anayoyaweka katika mtandao huo ni video, shoo anazozifanya na utayarishaji wa video za nyimbo zake.
Kutokana na idadi hiyo ya watazamaji, marioo amewaacha mbali baadhi ya wasanii wa Afrika wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki.