
Baada ya kuachia cover ya album yake mpya iitwayo “The Kid You Know” anayotarajia kuitoa Desemba 9, 2022, mwimbaji wa Bongofleva Marioo ametangaza kuwa ataachia historia fupi ya maisha yake kabla ya ujio wa album yake mpya.
Marioo ameeleza hilo kupitia insta story yake. Pia amebainisha kwa sasa unaweza ukai Pre-Order “The Kid You Know” kupitia Africori.
Album hiyo ya Marioo itakuwa na jumla ya nyimbo 18, huku nyimbo 3 toka kwenye album hiyo tayari zimeshatoka ambazo ni “Mi Amor”, “Naogopa” pamoja na “Dear EX”, nyimbo 15 zilizobaki zote ni mpya.