
Hitmaker wa Beer Tamu, Marioo ametangaza ujio wa tour yake nchini Tanzania aliyoipa jina la “I’am Marioo tour.”
Marioo ameweka wazi ujio wa tour yake hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwaachia mashabiki swali kupendekeza ni mkoa gani nchini Tanzania ambao asiache kukanyaga kwenye tour yake hiyo.
Pamoja na kuweka wazi ujio wa tour yake hiyo marioo hajagusia endapo kuna wasanii wengine ambao anatarajia kushirikiana nao kwenye tour hiyo au atakuwa mwenyewe tu.
Kauli ya marioo inakuja siku chache baada ya kuwatolea uvivu wasanii wa bongo fleva kwa kuwaita wanafiki pale linapokuja suala la kupeana michongo ya kufanikiwa kwenye muziki