Entertainment

MARTHA MUKISA ASHTAKIWA KWA WIZI WA WIMBO

MARTHA MUKISA ASHTAKIWA KWA WIZI WA WIMBO

Mwanamuziki Martha Mukisa ameingia kwenye headlines nchini Uganda mara baada ya kutuhumiwa kuiba wimbo wa wasanii wa kundi la VTS Boys.

Kulingana na wasanii hao Martha Mukisa aliimba mashairi yote ya wimbo wao uitwao “Its You” na kisha akaubadilisha jina kuwa “Ntibula” bila ridhaa yao baada ya kuuziwa wimbo huo na Nick Mulla ambaye aliwaandikia wimbo wao wa “Its You.”

Wasanii hao wamehoji kuwa Martha Mukisa anafahamu kabisa wimbo huo ni wao ila ameamua kupuuza kuhusu hakimiliki ya kazi hiyo.

Hata hivyo Martha Mukisa hajajibu kuhusu tuhuma za kuiba wimbo wa kundi la VTS Boys ila wasanii hao wametishia kumchukulia hatua kali za kisheria iwapo hatakata kuwalipa miraba ya wimbo wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *