LifeStyle

Marya Aibua Matumaini Mapya Kwa Mashabiki Wake Baada ya Stroke

Marya Aibua Matumaini Mapya Kwa Mashabiki Wake Baada ya Stroke

Mwanamuziki Marya, anayejulikana kwa kibao kilichotikisa ‘Chokozza’, ameonyesha maendeleo ya kuridhisha katika safari yake ya kupona baada ya kupata ugonjwa wa kupooza (stroke) uliomweka kitandani kwa muda.

Katika video mpya iliyoenea mitandaoni, Marya anaonekana akiwa mwenye furaha tele huku akisaidiwa kupata huduma ya pedicure na manicure katika kituo cha urembo cha Phoina Beauty. Hii imewapa mashabiki wake matumaini mapya juu ya safari yake ya kupona.

Marya aligundulika kuwa na tatizo hilo mwezi Mei mwaka 2025, baada ya habari hizo kufichuliwa kwa umma na mwimbaji mwenzake Avril, ambaye aliwahi kushirikiana naye kutengeneza wimbo wa ‘Chokozza’ uliopendwa sana kote nchini. Stroke hiyo ilimuathiri vibaya upande mzima wa mwili wake na kumfanya awe kwenye uangalizi maalum wa nyumbani.

Tangu wakati huo, Marya amekuwa akipokea huduma za uangalizi wa karibu ili kusaidia kurejesha uwezo wake wa kutumia viungo vyote vya mwili. Video yake ya hivi karibuni imewapa mashabiki na marafiki wake matumaini makubwa kwamba nyota huyo anaendelea kupata nafuu na huenda akarudi tena kwenye jukwaa la burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *