
Mwanamuziki Brown Mauzo amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya baby mama wake Vera Sidika kukiri kufanya upasuaji wa kupunguza makali yake kutokana na matatizo ya kiafya.
Kupitia mtandao wa Instagram ameandika waraka mrefu akipongeza mrembo huyo kwa hatua ya kujitokeza wazi na kuweka mapungufu yake kwa umma huku akisema itakuwa funzo kwa wadada ambao kwa njia moja au nyinngine wataka kubadilisha miili yao kwa upasuaji.
Katika hatua nyingine Mauzo amekiri kutamani maungo ya mrembo huyo kabla hajafanyiwa surgery ambapo ameenda mbali zaidu na kuhapa kwamba hatokuja kumkimbia Vera Sidika kutokana na muonekano wake mpya kwani alivutiwa na utu wake.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wametafsiri ujumbe huo wa Brown Mauzo kuwa ni njia msanii huyo kutengeneza mazingira ya kuachia wimbo mpya huku wakienda mbali zaidi na kuhoji kuwa hatua vera sidika kutangaza hadharini kufanya upasuaji wa kupunguza makalio ilikuwa ni mkakati wa kumtoa kisanaa.
Utakumbuka Brown mauzo na Vera Sidika ambaye walihalalisha mahusiano yao Septemba, 24 mwaka wa 2020 wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Amina Brown.