Gossip

Mashabiki Wamkosoa Bahati kwa Kuuonyesha DM ya Marehemu Shalkido

Mashabiki Wamkosoa Bahati kwa Kuuonyesha DM ya Marehemu Shalkido

Msanii Bahati amekosolewa vikali na mashabiki mitandaoni baada ya kushiriki picha ya ujumbe wa DM kutoka kwa marehemu msanii wa Gengetone, Shalkido, aliyeaga dunia hivi karibuni.

Kwenye screenshot aliyochapisha, Shalkido alikuwa akimuomba Bahati kufanya kolabo au kumunganisha na mkewe Diana Bahati ili waweze kushirikiana katika wimbo. Hata hivyo, kilichowakasirisha mashabiki wengi ni kwamba Bahati hakuwahi kujibu ujumbe huo.

Mashabiki wameonyesha masikitiko na hasira, wakimtuhumu Bahati kwa kutafuta kiki badala ya kuonyesha utu na huruma.
Wengi walihoji kwa nini ameamua kuonyesha ujumbe huo baada ya kifo cha Shalkido, ilhali hakuchukua hatua yoyote alipokuwa hai.

Wengine walimtaja Bahati kuwa mnafiki na asiye na hisia, wakisema alipaswa kutumia ushawishi wake kumuinua Shalkido wakati alipokuwa angali hai, badala ya kuonekana kama anatafuta umaarufu kupitia kifo chake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *