
Msanii nyota wa Bongo Fleva, Mbosso, amefunguka kuhusu namna alivyoweka nguvu kubwa kuhakikisha onyesho lake kwenye Simba Day linakuwa la kipekee, akieleza kuwa nusra ajitoe uhai wake ili kuwafurahisha mashabiki wa Simba Sports Club.
Kupitia Instagram, Mbosso amesema alijiandaa kwa moyo wake wote na kuweka nguvu, muda na rasilimali nyingi kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Amebainisha kuwa mapenzi yake kwa Simba SC na mashabiki wake ndiyo yaliyomsukuma kufanya maandalizi ya hali ya juu, akisisitiza kuwa alijitolea zaidi ya kawaida ili burudani iwe ya kukumbukwa.
Licha ya mafanikio makubwa ya perfomance yake, msanii huyo pia amewaomba mashabiki na viongozi wa Simba SC msamaha endapo kulikuwa na mapungufu yoyote katika utendaji wake wa Kazi, akisema yeye ni mwanadamu na hawezi kufanya kila kitu kwa ukamilifu.
Simba Day hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuzindua msimu mpya wa klabu hiyo yenye mashabiki wengi, na mwaka huu Mbosso alipewa nafasi ya kuwa headliner, nafasi ambayo amesema itaendelea kubaki kuwa kumbukumbu muhimu katika maisha yake ya muziki.