Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso, ameandika historia mpya katika safari yake ya muziki baada ya kufikisha jumla ya watazamaji (views) bilioni 1 kwenye mtandao wa YouTube kupitia nyimbo zake zote.
Mbosso alijiunga rasmi na YouTube tarehe 2 Novemba mwaka 2017, na tangu wakati huo amekuwa akitoa kazi zilizopokelewa vyema na mashabiki wake ndani na nje ya Afrika Mashariki. Mafanikio haya yanaonesha ukuaji mkubwa wa umaarufu wake pamoja na mvuto wa muziki wake katika soko la kimataifa.
Kupitia hatua hii, Mbosso ameingia kwenye orodha ya mastaa wachache wa Tanzania waliowahi kufikisha views bilioni 1 YouTube, akijiunga na majina makubwa kama Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize na Rayvanny.
Mafanikio ya Mbosso yanaendelea kuthibitisha mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa Bongo Fleva na kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa, huku mashabiki wake wakimpongeza kwa kazi nzuri na bidii kubwa tangu alipoanza safari yake ya muziki.