Msanii wa nyota wa Bongo Flava, Mbosso, amekanusha vikali madai yanayosambaa mitandaoni yanayodai kuwa amemkimbia meneja mkubwa Fella Sweet Fella katika kipindi ambacho meneja huyo anaumwa.
Akizungumza kuhusu taarifa hizo, Mbosso amesema madai hayo si ya kweli, akiyataja kuwa ya kupotosha umma. Amesema amekuwa karibu na familia ya Mkubwa Fella, akiwatembelea mara kwa mara, pamoja na kutoa msaada wowote unaohitajika kadri ya uwezo wake.
Mbosso amesisitiza kuwa anamthamini sana Mkubwa Fella kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika safari yake ya muziki na hawezi kamwe kumsahau wala kumtelekeza kama baadhi ya walimwengu wanavyodai.
Hata hivyo, hitmaker huyo wa Pawa, ameomba umma na mashabiki kupuuza taarifa zinazolenga kuchafua jina lake ikizingatiwa kuwa Mkubwa Fella alikuwa moja kati ya watu ya waliyoikuza kipaji chake na kumtambulisha kwa mashabiki wengi wa muziki ndani na nje ya Tanzania chini ya Yamoto Band.