Entertainment

Mbosso Kuachia Version Tatu za “Pawa” Kutoka Kenya, Tanzania na Rwanda

Mbosso Kuachia Version Tatu za “Pawa” Kutoka Kenya, Tanzania na Rwanda

Mwanamuziki nyota wa Bongofleva, Mbosso, ametangaza kuwa anajiandaa kuachia version tatu tofauti za wimbo wake “Pawa,”. Kila version itawashirikisha wasanii wakubwa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki hasa mataifa ya Kenya, Tanzania na Rwanda

Katika version ya Kenya, Mbosso amewashirikisha nyota wawili, Bien wa Sauti Sol na mfalme wa rap nchini Kenya, Khaligraph Jones.
Toleo la Tanzania linakuja na nguvu ya Darassa, Billnass na Marioo, wasanii wanaosifika kwa uandishi, mitiririko na ubora wa midundo ya Bongo Fleva.

Kwa upande wa Rwanda, Mbosso ameungana na The Ben, mmoja wa wanamuziki bora na wenye sauti yenye utamu katika ukanda huo.

Mbosso amedokeza kuwa huenda akaachia version zaidi ya tatu, akiwashirikisha wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki kutokana na mapokezi makubwa ya wimbo huo.

“Pawa” ni wimbo uliopata mafanikio makubwa kutoka kwenye EP yake Room 3, na remix hizi zinatarajiwa kuufikisha mbali zaidi kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *