Entertainment

Mbunge Babu Owino Afurahi Kukutana na Rapa Kaycyy

Mbunge Babu Owino Afurahi Kukutana na Rapa Kaycyy

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, ameonyesha furaha yake kubwa baada ya kukutana na mshindi wa tuzo za Grammy mwenye asili ya Kenya, Rapa KayCyy, ambaye amerejea nchini humo baada ya kukaa Marekani kwa zaidi ya miaka 17.

Owino, ambaye anamezea mate kiti cha ugavana wa Nairobi mwaka 2027, amesema KayCyy ni miongoni mwa vipaji muhimu ambavyo Kenya inahitaji kuleta mabadiliko makubwa yanayolenga kuifanya Nairobi kuwa jiji lenye ushindani wa kimataifa.

Mbunge huyo, ameongeza kuwa wanatamani kumpa msanii huyo nafasi ya kuonyesha mchango wake katika mustakabali wa kaunti ya Nairobi na taifa kwa ujumla.

KayCyy, anayeheshimika kwenye anga za muziki wa kimataifa, amechangia pakubwa mafanikio ya albamu ya DONDA ya Kanye West iliyoshinda Tuzo ya Grammy. Lakini pia ameshirikiana na wasanii wakubwa kama Lil Baby, Lil Wayne na Travis Scott, hatua iliyompa umaarufu mkubwa katika muziki wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *