Mshereheshaji na mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Emmanuel Mathias, anayefahamika zaidi kama MC Pilipili, amefariki dunia leo Novemba 16, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa tulizozipokea muda huu, MC Pilipili alikuwa safarini kuelekea jijini Dodoma, ambako alitarajiwa kufanya kazi ya ushereheshaji jioni ya leo. Hata hivyo, akiwa njiani, alifariki dunia ghafla kabla ya kufikishwa hospitalini.
Taarifa hizi zimethibitishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General ya Dodoma, Dkt. Ernest Ibenzi, ambaye amesema kuwa MC Pilipili alifikishwa hospitalini tayari akiwa ameshafariki dunia. Hadi sasa chanzo cha kifo chake hakijafahamika, na uchunguzi unaendelea.
Kifo cha MC Pilipili kimetamausha wengi, wakiwemo mashabiki, wasanii wenzake na wadau wa tasnia ya burudani, ambao kwa sasa wanaendelea kutuma salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.
MC Pilipili anabaki kukumbukwa kwa ucheshi wake, karama yake ya kuwatia watu faraja, na mchango wake mkubwa katika sanaa ya uigizaji na ushereheshaji nchini Tanzania.
Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.