Entertainment

Otile Brown Aachia Tracklist ya EP yake Mpya

Otile Brown Aachia Tracklist ya EP yake Mpya

Msanii mahiri wa RnB kutoka Kenya, Otile Brown, ametangaza rasmi orodha ya nyimbo za EP yake mpya inayokwenda kwa jina “The Real King of the East”. EP hii ina jumla ya ngoma tano kali na imebeba kolabo tatu za uzito zinazomshirikisha Jovial, The Ben, na Okello Max.

Katika mradi huo, Otile amemshirikisha The Ben katika wimbo “For Life”, akamleta Jovial kwenye ngoma “I Choose You”, na kisha Okello Max katika wimbo “I Love You”. Aidha, EP inajumuisha pia wimbo “Miss the Water” pamoja na “Lala Salama Baba”, ambao ni wimbo wa kumkumbuka na kumuenzi Raila Odinga.

EP ya “The Real King of the East” inatarajiwa kuingia sokoni Novemba 21, 2025, na tayari mashabiki wanaonyesha msisimko mkubwa wakisubiri kusikia mwelekeo mpya wa Otile Brown kupitia kazi hii mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *