Entertainment

Eric Omondi afunguka baada ya kutupiwa lawama za usaliti

Eric Omondi afunguka baada ya kutupiwa lawama za usaliti

Mchekeshaji maarufu Afrika Mashariki na kati Eric Omondi amefunguka baada ya kutupiwa lawama za usaliti baada ya kucheza wimbo wa Diamond Platnumz, Chitaki.

Kwenye mahojiano na Mungai Eve amesema hajutii kitendo cha kumuonyesha upendo bosi huyo wa WCB kwa kusema kwamba alikuwa anajaribu kuondoa kasumba ya watu kumchukulia kuwa anawachukia wasanii wa kigeni.

Aidha amesisitiza kuwa bado ataendelea kujitoa mhanga kupigania tasnia ya muziki nchini kwa kushinikiza asilimia 75 za nyimbo za kenya zipigwe kwenye vyombo vya habari.

Lakini pia amezungumzia kolabo ya Stevo Simple Boy na Ruger wa Nigeria kwa kusema wimbo wa wawili hao huenda ukaachia mwakani ikizingatiwa kuwa uongozi wa wasanii hao wawili tayari wameanza mazungumzo ya kufanikisha kolabo yao.

Kauli ya Omondi imekuja mara baada ya jana Ruger kumkataa hadharani msanii huyo wa Men In Business kuwa hamfahamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *