Entertainment

Mchekeshaji Eric Omondi Atangaza Nia ya Kugombea Nafasi ya Kisiasa 2027

Mchekeshaji Eric Omondi Atangaza Nia ya Kugombea Nafasi ya Kisiasa 2027

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii, Eric Omondi, ametangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi ya kisiasa kama Mwakilishi wa Vijana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, hatua inayoongeza orodha ya wasanii wanaoingia katika ulingo wa siasa nchini Kenya.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Omondi amesema kuwa ushiriki wa vijana katika mchakato wa kupiga kura ni jambo la msingi endapo Kenya inataka kushuhudia mabadiliko ya kweli. Amesisitiza kuwa vijana wana nguvu kubwa ya kuamua hatima ya nchi, hivyo wanapaswa kuchukua nafasi za uongozi badala ya kuachwa pembeni.

Mchekeshaji huyo amefichua kuwa iwapo atachaguliwa, atashinikiza mabadiliko makubwa ya kikatiba baada ya uchaguzi, yakiwemo mapendekezo ya kupunguza idadi ya kaunti pamoja na kuondoa baadhi ya nyadhifa za kuchaguliwa, akisema hatua hizo zitapunguza gharama za uendeshaji wa serikali na kuleta ufanisi.

Hata hivyo, Eric Omondi amewakosoa vikali baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kile alichokitaja kuwa ni kuwadhalilisha na kuwadharau vijana, akiongeza kuwa matukio ya hivi karibuni nchini Kenya yanaonyesha wazi dhana potofu inayotumiwa dhidi ya vijana licha ya mchango wao mkubwa katika maendeleo ya taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *