Gossip

Mchekeshaji Nasra Yusuf Apigwa Block na Zuchu Instagram Kisa Maandamano Tanzania

Mchekeshaji Nasra Yusuf Apigwa Block na Zuchu Instagram Kisa Maandamano Tanzania

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Nasra Yusuf, amedai kwamba msanii wa Bongo Fleva Zuchu amempiga block kwenye mtandao wa Instagram.

Nasra amesema hatua hiyo imekuja baada ya yeye kushinikiza wasanii wa Tanzania kuzungumza wazi kuhusu hali ya maandamano na ukatili unaoripotiwa nchini humo.

Kwa mujibu wa Nasra, lengo lake lilikuwa kuwataka mastaa kutumia ushawishi wao kukemea maovu yanayowakumba wananchi, lakini kauli yake haikupokelewa vyema na baadhi ya wasanii, akiwemo Zuchu.

Tukio hili limezua mijadala mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wameunga mkono msimamo wa Nasra, huku wengine wakimtetea Zuchu wakisema hana wajibu wa kutoa maoni ya kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *