
Rapa kutoka nchini Marekani, Meek Mill ameamua kuichana Lebo yake kwa kile anachodai kwamba haijamlipa pesa zake zilizotokana na muziki wake kuuzwa.
Kupitia mfululizo wa tweets zake kwenye mtandao wa Twitter Meek Mill amesema hajalipwa na hafahamu ni kiasi gani cha pesa lebo yake imeingiza kutoka kwenye muziki wake ambapo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba anahitaji Mwanasheria wa kumtetea ili aweze kupata haki yake.
Hakuishia hapo, Meek Mill ametishia kuanika wazi mkataba wake ifikapo Jumatatu ijayo ili dunia ione udhalimu wa lebo yake.
Hata hivyo Meek Mill ambaye anasimamiwa na Roc Nation, hajaweka wazi jina la Label ambayo anaituhumu, kama ni Maybach Music Group au Atlantic Records