
Rapa kutoka nchini Marekani Meek Mill ametangaza kurudi tena barani Afrika kwa mara ya pili baada ya kutua kwa mara ya kwanza nchini Ghana kwenye tamasha la Afro Nation lililofanyika mwishoni mwa mwaka 2022
Meek ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa anatarajia kutua nchini Nigeria muda wowote kuanzia sasa.
“Nakuja Nigeria”, Aliandika.
Lakini pia Rapa huyo amefunguka kuwa anahitaji msambazaji wa kazi zake Barani Afrika na Uingereza. Si hivyo tu Meek amesisitiza kuwa Afrika ni Bara kubwa zaidi duniani, inabidi watu tujiunge kwa pamoja