Entertainment

Meek Mill awatoa jela wanawake 20 huko Philadelphia

Meek Mill awatoa jela wanawake 20 huko Philadelphia

Rapa Meek Mill ambaye alizaliwa na kukulia mjini Philadelphia, Marekani ameamua kurudisha fadhila kwao.

Rapa huyo ameripotiwa kuwatoa wanawake 20 jela huko Philadelphia kwa kuwalipia dhamana zao. Lengo la Meek Mill kufanya hivyo, ni kuhakikisha kuwa wanarudi nyumbani kufurahia sikukuu na familia zao.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Meek Mill amesema “Ilikuwa ni huzuni kwangu kuwa mbali na mwanangu katika kipindi cha sikukuu wakati nilipokuwa jela…hivyo ninaelewa wanachopitia wanawake hawa na familia zao, hakuna mtu anayepaswa kukaa gerezani kwa sababu tu hana uwezo wa kulipa dhamana.

“Nashukuru kupata nafasi ya kuwasaidia wanawake hawa kuwa pamoja na familia zao katika msimu huu maalum wa mwaka”

Tayari wanawake 5 wameachiwa kutoka jela lakini 15 wengine wanatajwa kuachiwa huru wiki ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *