
Rapa kutoka Marekani Megan Thee Stallion ameendelea kufunguka ambayo hatuyafahamu kwenye shtaka lake la kupigwa risasi ya mguu na Tory Lanez Julai 12 mwaka 2020 Jijini Los Angeles.
Televisheni ya CBS imeachia mahojiano yote ya Megan Thee Stallion ambapo mrembo huyo amesikika kwamba Tory Lanez alijaribu kumuonga na shilling million 115 za kenya ili asiwaambie polisi kuwa ndiye aliyempiga risasi.
“Aliomba radhi, alisema samahani sana tafadhali usimwambie mtu yeyote, nitakupatia ‘Dola Milioni’ kama hutosema chochote.” alieleza Megan Thee Stallion kwa uchungu huku akifuta machozi.
Aprili 6 mwaka huu Tory Lanez aliachiwa kwa dhamana ya shilling milllioni 40 za Kenya baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka amri ya mahakama iliyotolewa kumkinga Megan Thee stallion kwenye shtaka lao linaloendelea.
Ikumbukwe Tory Lanez anakabiliwa na Mashtaka mawili ambayo ni kumshambulia rapa Megan thee Stallion mwaka 2020 na pia kubeba silaha yenye risasi kinyume na sheria.