Entertainment

Mejja ataka bangi kuhalalishwa Kenya

Mejja ataka bangi kuhalalishwa Kenya

Mwanamuziki nyota nchini Mejja ametaka serikali kuhalalisha kilimo cha mimea wa bangi kwa manufaa ya taifa.

Kwenye mahojiano na Plug tv Hitmaker huyo wa Kanairo Dating amesema licha ya bangi kuwa na mitazamo hasi katika jamii, serikali inapaswa kuja na mkakati wa kuhakikisha kuwa zao hilo linazalisha pato la taifa.

Kauli ya mejja imekuja mara baada ya Rapa Octopizzo miezi miwili iliyopita kumtaka Rais William Ruto kuihalalisha bangi pindi tu atakapokula kiapo cha kuingia ofisini kama Rais wa tano wa Kenya.

Katika video ambayo ilisambazwa mitandaoni, Octopizzo alimuelezea Ruto kwamba hata kama ataona kuhalalisha bangi ni jambo gumu basi aifanye isiwe kama ni hatia kwa mtu anayepatikana naye bali liwe tu ni jambo la kawaida.

“Najua wewe ni mkristo na kwa hiyo hili gumzo huenda litakuwa gumu kidogo kwako lakini unajua bangi ni moja ya dawa ambazo ni takatifu zaidi duniani. Na amabcho nakuomba hata si kuhalalisha matumizi yake bali ni kuiweka bangi isiwe kama hatia kwa mtu anayepatikana nayo,” alisema Octopizzo.

“Juzi nilikuona ulikutana na seneta wa Delaware, huko mtu anaruhusiwa kutembea na bangi gramu 3 kwa kujivinjari tu ilmradi mtu ako na miaka 21. Hii ni biashara ya mabilioni na tunajua kuna watu serikalini wenye wanafanya biashara hiyo,” Staa huyo alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *