
Meneja kutoka lebo ya muziki ya 001 Music Mangisi amepuzilia mbali madai ya msanii Happy C kuuza gari lake baada ya walimwengu kuhoji ametoswa na bosi wa lebo hiyo Hassan Joho.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mangisi amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwani happy c bado anaendelea kupata msaada kutoka kwa gavana huyo wa zamani wa kaunti ya mombasa.
Mangisi amekazia kuwa kuondoka kwa Hassan Joho mamlakani hautamrudisha nyuma kimuziki msanii Happy C kwa sababu ana imani kuwa Joho atamsaidia hata akiwa nje ya siasa.
Kauli yake imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kudai kuwa huenda Happy C ameuza gari lake kwani mara kwa mara amekuwa akitumia usafiri wa boda boda kwenye shughuli zake.