Entertainment

Meneja wa Spice Diana atuhumiwa kumtishia mtu maisha Uganda

Meneja wa Spice Diana atuhumiwa kumtishia mtu maisha Uganda

Mcheza densi kutoka Uganda Ritah amejitokeza na kumshutumu meneja wa msanii Spice Diana, Roger Lubega kwa kumtishia maisha.

Ritah anasema Roger na timu yake wamekuwa wakimtumia jumbe za vitisho kuwa watamtoa uhai kutokana na matamshi yake dhidi ya tamasha la Spice Diana lililofanyika juzi kati huko Lugogo Cricket Oval.

Ritah alidai enesho la Spice Diana halikuwa na mvuto, jambo ambalo lilimkasirisha Roger Lubega.

“Marafiki zangu, nina hofia maisha yangu. Kama kuna jambo lolote litanitokea, mnajua wa kuwalaumu. Wale jamaa ni hatari kama mnavyofahamu, huko nyuma wamekuwa wakihusishwa na mauaji. Siwezi kuchukua vitisho vyao kwa wepesi,” alisema.

Julai mwaka jana, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Henry Nsamba, aliuawa nyumbani kwa Spice Diana eneo la Makindye na tangu kipindi hicho familia ya mwenda zake hajawahi pata haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *