Entertainment

Meneja wa Stevo Simple Boy Adaiwa Kumdhulumu Kifedha, Wakili Aingilia Kati

Meneja wa Stevo Simple Boy Adaiwa Kumdhulumu Kifedha, Wakili Aingilia Kati

Msanii maarufu wa muziki nchini Kenya, Stevo Simple Boy, amezua gumzo tena baada ya yeye na mkewe Brenda kufanya ziara kwa Mfanyibiashara Sarah Mtalii na kufunguka kuhusu changamoto zinazomkumba msanii huyo hasa kuhusu usimamizi wake wa kazi.

Katika mahojiano hayo, Brenda alionyesha masikitiko makubwa kuhusu namna ambavyo Stevo anavyotendewa na meneja wake, Machabe Geoffrey. Brenda alidai kuwa licha ya Stevo kufanya maonyesho ya bei ya ghali, bado hana uwezo hata wa kujikimu kimaisha.

Brenda alisema: “My issue is Stevo namtetea apate haki yake vizuri. Juu management ako nayo ni kama inamtesa. So my main point is, Stevo ameshinda akifanya kazi na meneja wake anaitwa Machabe Geofrey na hana hata one bob. Unapata ameenda show ya 80,000 lakini anarudi hana hata shillingi. Hajui hata pesa imeenda wapi?”

Wakati wa mazungumzo hayo, Sarah Mtalii alimuuliza Stevo kama anatumia pesa kwa anasa au mihadarati, lakini msanii huyo alikanusha vikali.

 Stevo alijibu: “Hapana, mimi si mtu wa sherehe, situmii mihadarati. Mimo niko vile unaniona hivi. Meneja ndiye anapokea pesa za shows na nikimuuliza kuhusu account, anasema ataniambia baadaye.”

Kwa sasa, familia ya Stevo imetafuta msaada wa kisheria na wakili Mwenda Njagi ameanza hatua za kumsaidia Stevo kupata haki yake na kudhibiti mapato yake kama msanii.

Taarifa hii imeibua hisia mseto mitandaoni huku mashabiki wakitaka meneja huyo ajibu tuhuma hizo. Wengi wameonyesha kumuunga mkono Stevo na kumtakia mafanikio katika safari yake ya kurejesha udhibiti wa maisha yake ya kisanii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *