
Mfumo wa uendeshaji wa Android umeleta mabadiliko ya kuvutia katika sehemu ya call-screen, sehemu inayowaonesha watumiaji picha na taarifa wakati mtu anapopigia simu. Mabadiliko haya yanajumuisha mfumo mpya unaoitwa “Calling Card”, ambao umeboresha kabisa uzoefu wa kupokea simu.
Kwa mfumo huu mpya wa Calling Card, picha ya mpigia simu sasa inaonekana kwa ukubwa wa skrini nzima (full screen) na kwa mtindo wa kisasa zaidi unaowezesha mtumiaji kuchagua ni picha gani anayotaka ionekane pale anapopigiwa simu. Zaidi ya hayo, mtumiaji anaweza kubadilisha maandishi yanayohusiana na jina la mpigia simu pamoja na rangi za maandishi hayo, hivyo kufanya mwonekano kuwa wa kipekee na wa kibinafsi.
Mabadiliko haya yanatoa uhuru zaidi kwa watumiaji wa Android kuunda uzoefu wa simu unaoendana na ladha zao na mitindo wanayopendelea, na kuifanya sehemu ya kupokea simu kuwa ya kuvutia zaidi na rahisi kutumia.
Kwa sasa, mabadiliko haya yameanza kuletwa kwa baadhi ya watumiaji na yanatarajiwa kufikia simu nyingi zinazotumia mfumo wa Android kwa hatua kwa hatua katika siku zijazo.