LifeStyle

Ellah Aachana Rasmi na Mzazi Mwenzake Steve Odek

Ellah Aachana Rasmi na Mzazi Mwenzake Steve Odek

Ellah Ray, dada yake sosholaiti maarufu Amber Ray, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kutangaza kuvunja uhusiano wake na baba wa mtoto wake, Steve Odek, huku akimshtumu kwa usaliti na mahusiano ya siri na wanawake kadhaa jijini Nairobi, akiwemo mwigizaji Jackie Matubia.

Kupitia mfululizo wa jumbe za hisia kwenye Insta Story, Ellah alisema hatimaye amefikia kikomo baada ya kuvumilia zaidi ya miaka mitatu ya kile alichokiita kudhalilishwa, kutopewa heshima na usaliti wa mara kwa mara. Alifichua kuwa kwa muda mrefu alijikuta akibeba maumivu kimya kimya na kuendelea kusimama na Odek licha ya onyo nyingi alizopewa.

Ellah aliongeza kuwa anajutia hatua yake ya kumtetea mpenzi wake wa zamani, hali iliyomfanya hata kupoteza uhusiano mzuri na baadhi ya wanafamilia wake kwa sababu ya kumlinda.

Kufuatia madai hayo, mitandao ya kijamii imewaka moto huku mashabiki wakitoa maoni tofauti, wengine wakimuunga mkono kwa ujasiri wake wa kusema ukweli, na wengine wakisubiri majibu ya wale waliotajwa kwenye sakata hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *