
Aliyekuwa msaidizi wa mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu Sean “Diddy” Combs, anayejulikana kwa jina la Mia, amejitokeza mahakamani kutoa ushahidi mzito unaomhusisha mwajiri wake wa zamani na unyanyasaji wa kingono.
Mia alieleza mbele ya mahakama jinsi alivyodhalilishwa kingono na Diddy, akisema tukio hilo lilimuacha akiwa na hofu kubwa, aibu na maumivu ya kihisia ambayo bado hayajapona. Alisema kuwa tukio hilo lilikuwa la kutisha na kwamba alihisi hana njia ya kujitetea wala kuondoka katika mazingira hayo.
Katika ushahidi wake, Mia alifunguka kuhusu hali ya uoga aliyokuwa nayo wakati huo, akihisi kuwa hangeweza kusema ukweli kwa kuhofia athari za kazi na maisha yake. Alisema aliishi kimya kwa muda mrefu kabla ya kupata ujasiri wa kusimulia yaliyomtokea.
Kesi dhidi ya Diddy imeendelea kupata uzito huku mashahidi kadhaa wakijitokeza na madai mbalimbali, yote yakionyesha taswira tofauti ya mtu ambaye kwa muda mrefu ameonekana kama miongoni mwa majina makubwa kwenye muziki na biashara ya burudan
Kesi hii imeongeza moto kwenye mjadala unaoendelea kuhusu nguvu, hofu, na unyanyasaji katika sekta ya burudani, hasa ikizingatiwa kuwa Diddy ni mmoja wa majina makubwa kwenye tasnia hiyo. Hata hivyo, Diddy hajatoa tamko rasmi kuhusu madai haya mapya, lakini mawakili wake wamekanusha tuhuma zote zilizowahi kuibuliwa dhidi yake katika kesi nyingine.