
Msanii wa kike nchini Miss P amefunguka na kudai kuwa hatawahi fanya collabo tena na msaani mwenzake Willy Paul hadi mwisho wa dunia.
Miss P ametujuza hayo kupitia ukurasa wake wa instagram alipomjibu shabiki yake aliyemuomba wafanya kollabo tena na Willy Paul kwa kusema “Naheshimu sana mawazo yako shabiki yangu ila hutokaa uje tena kusikia kollabo hiyo.”
Miss P na Willy P walishawahi kufanya kolabo kupitia nyimbo kama Liar, Fall in Love na Mashallah zilizotoka mwaka wa 2021 lakini walikuja wakaingia kwenye ugomvi mwishoni mwa mwaka jana baada Miss P kujitokeza na kudai kwamba aliondoka kwenye lebo ya muziki ya saldido International kwa sababu alinyanyaswa kimapenzi na willy paul ambaye ndiye mmiliki wa lebo hiyo.