Gossip

Mjakamfine Amzawadi Mokaya PlayStation 5 ya Laki Moja ya Kenya

Mjakamfine Amzawadi Mokaya PlayStation 5 ya Laki Moja ya Kenya

Msanii wa vichekesho nchini Kenya, Mjaka Mfine, ameonyesha mapenzi ya dhati kwa kumzawadia mpenzi wake aiitwaye Mokaya kifaa cha kisasa cha michezo ya video, PlayStation 5, chenye thamani ya takribani shilingi laki moja za Kenya.

Zawadi hiyo imetokana na ubashiri wa Mokaya uliotimia baada ya kudai kuwa klabu ya Manchester City ingeilaza Real Madrid katika mchezo wa Klabu Bingwa Barani Ulaya uliochezwa Desemba 10. Baada ya matokeo kuthibitisha alichokiamini, mrembo huyo alitimiza ahadi yake kwa kumfurahisha mpenzi wake Mokaya kwa zawadi hiyo ya gharama kubwa.

Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo ilifanyika katika mazingira ya furaha na ilihudhuriwa na marafiki wa karibu pamoja na wasanii wenzake, ambapo Mokaya alionekana kufurahia sana zawadi aliyopokea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *