Gossip

Guardian Angel Awasisimua Mashabiki kwa Kumsuprise Mkewe kwa Lunch Maalum

Guardian Angel Awasisimua Mashabiki kwa Kumsuprise Mkewe kwa Lunch Maalum

Msanii wa muziki wa Injili, Guardian Angel, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuamua kumpa mke wake, Esther Musila, suprise ya kipekee kwa kumpeleka kwenye lunch maalum wakati walipokuwa jijini Kisumu kwa shughuli za kikazi.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Guardian ameposti video inayoonesha safari yao pamoja na nyakati za furaha walizoshiriki katika mkahawa mmoja huko Kisumu. Kwenye video hiyo, wawili hao wanaonekana wakifurahia vyakula mbalimbali huku wakicheka na kubadilishana mazungumzo ya upendo, hali iliyowavutia mashabiki wengi.

Hatua hiyo imefasiriwa na wengi kama ujumbe mzito kwa wanaume wa Kenya kuhusu umuhimu wa kuthamini na kuenzi wake zao, bila kujali mazingira au maoni ya watu wengine.

Guardian Angel pia anaonekana kupuuza kabisa ukosoaji uliowahi kujitokeza kuhusu kuoa mke aliyemzidi kiumri kwa kudhihirisha kuwa mapenzi ya kweli hayapimwi kwa umri bali kwa heshima, uelewano na upendo wa dhati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *