
Mke wa msanii Peter Miracle Baby, Carol Katrue amehapa kumfungulia mashataka baby mama wa msanii huyo kwa madai ya kuwakodisha watu wawaribie brand yao.
Katika mahojiano yake amesema baby mama huyo aitwaye Tash Baby amekuwa akiwalipa watu wawaribie jina kitu ambacho kimewapelekea kupoteza dili la shillingi millioni 1 kutokana na skendo ambazo zimekuwa zikiwafuata katika siku za hivi karibuni.
Kauli ya Carol Katrue imekuja mara baaada ya mrembo aitwaye Bree aliyedai kuwa ana uja uzito wa Peter Miracle Baby kujitokeza kwenye moja ya interview na kudai kuwa alilipwa shilling 3,500 na Tash Baby adanganye kuwa ana uja uzito wa msanii huyo