
Vanessa Bryant ambaye ni mke wa marehemu Kobe Bryant, amepatiwa fidia ya ($16 million) kufuatia tukio la kusambaza picha za miili ya marehemu mtandaoni baada ya ajali ya helikopta ambayo ilichukua uhai wa mumewe, binti yake pamoja na wengine 9.
Mahakama imejiridhisha kwamba Kitengo cha Zimamoto na ukoaji pamoja na Idara ya polisi wadogo Jijini Los Angeles walivunja haki ya faragha kwa kusambaza picha hizo za marehemu na kumsababishia Vanessa pamoja na wahanga wengine msongo wa mawazo.
Mbali na Vanessa Bryant, mlalamikaji mwingine aitwaye Chris Chester ambaye pia alipoteza mke na binti yake kwenye ajali hiyo iliyotokea February, 2020 naye amepatiwa kiasi cha ($15 million) ikiwa ni sehemu ya shauri lao la madai ya fidia kiasi cha ($31 million)