
Gwiji la Soka Duniani Edson Arantes do Nascimento maarufu kama PELE amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Kifo cha mwanasoka huyo, kimethibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye Instagram.
Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu mwaka 2021.
Pele anayetajwa kama miongoni mwa Wachezaji wa soka wa kipekee kuwahi kutokea Duniani amewahi kutwaa Kombe la Dunia mara tatu akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil.