Sports news

Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Todd Boehly ajiuzulu

Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Todd Boehly ajiuzulu

Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Todd Boehly ameripotiwa kujiuzulu wadhifa aliokuwa ameshikilia kikaimu kama msimamizi wa kutambua na kusajili wachezaji wapya katika timu hiyo.

Mwaka jana baada ya kuinunua timu hiyo kutoka kwa bilionea wa Urusi Roman Abrahamovic, Boehly alijitwika jukumu la kuwa mkurugenzi wa kuangalia na kusajili vipaji vipya katika Chelsea na inadiwa kuwa yeye ndiye aliongoza kusajiliwa kwa wachezaji kama Pierre Emerick Aubameyang, Marc Cucurela, Kalidou Koulibaly pamoja pia na kumfuta kazi kocha Thomas Tuchel na kumleta Muingereza Graham Potter.

Wadhifa wa msimamizi wa kusajili vipaji vipya Chelsea ulikuwa umeshikiliwa na Marina Granovskaia pamoja na golikipa mkongwe Peter Cech ambao wote walitangaza kuondoka pindi tu uongozi mpya ulipochukua hatamu kama wamiliki wa Chelsea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *