
Timu ya Taifa ya Morocco imeandika historia kubwa ulimwenguni baada ya kuitoa Hispania na kutinga Robo Fainali ya Kombe la Dunia 2022 mchujo Qatar.
Baada ya sare ya 0-0 ikicheza kwa kujilinda ndani ya dakika 120, Simba wa Atlasi walikwenda kushinda kwa penalti 3-0, shujaa akiwa na kipa Bono aliyeokoa penalti mbili za Sergio Busquets na Carlos Soler baada ya ile kwanza iliyopigwa na Pablo Sarabia kwenda nje.
Waliofunga penalti za Morocco ni Abdelhamid Sabiri, Badr Benoun na Achraf Hakimi na sasa Morocco Β itamenyana na Ureno kuibamiza Uswiss 6-1
Mshambuliaji kinda Goncalo Ramos aliyechukua nafasi ya nyota Cristiano Ronaldo aliyeanzia kwenye benchi katika mchezo huo, alifunga mabao matatu huku Pepe, Raphael Guerreiro na Rafael Leao wakifunga bao moja kila mmoja katika ushindi huo mujarabu.
Beki Manuel Akanji alifungia Uswizi bao la pekee la kufuta machozi.