Entertainment

Mr Eazi Afunga Ndoa na Temi Otedola Katika Harusi ya Kifahari Iceland.

Mr Eazi Afunga Ndoa na Temi Otedola Katika Harusi ya Kifahari Iceland.

Mwanamuziki kutoka Nigeria, Mr Eazi, amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Mwigizaji Temi Otedola, katika sherehe ya kifahari iliyosheheni usiri mkubwa, iliyofanyika nchini Iceland.

Harusi hiyo ilifanyika Ijumaa, tarehe 8 Agosti 2025, ndani ya Kanisa maarufu la Hallgrímskirkja lililopo mjini Reykjavik. Tukio hilo lilihudhuriwa na familia na marafiki wa karibu pekee, akiwemo mama yake bi harusi, Nana Otedola, na dada yake, DJ Cuppy.

Miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria ni tajiri namba moja barani Afrika, Bilionea Aliko Dangote, ambaye alishuhudia kiapo cha wawili hao waliodumu kwenye mahusiano tangu mwaka 2017.

Harusi hiyo imezua gumzo mitandaoni kutokana na uzuri wa mandhari ya Iceland na umakini uliowekwa kuhakikisha inabaki kuwa tukio la kifamilia, likithibitisha kwamba mapenzi ya kweli hayahitaji hadhira kubwa ili kung’aa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *